728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, September 18, 2016

    KOCHA WA REAL MADRID ATUPIWA VIRAGO MOROCCO

    .

    John Toshack

    Casablanca,Morocco.

    BAADA ya kukishuhudia kikosi chake kikilala kwa mabao 4-0 toka kwa Zamalek ya Misri katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya nusu fainali ya michuano ya klabu bingwa Afrika Ijumaa Usiku katika dimba la uwanja wa Borg El Arab,Alexandrid,Wydad Casablanca,imemtimua kazi aliyekuwa kocha wake Mkuu,John Toshack.

    Taarifa iliyochapishwa katika tovuti rasmi ya klabu hiyo imesema Wydad Casablanca imeamua kuvunja mkataba na Toshack baada ya kuchukizwa na kichapo hicho cha Ijumaa Usiku.

    Ikumbukwe kabla ya kufungwa na Zamalek,Toshack,alikuwa ameshindwa kuipa ushindi Wydad Casablanca katika michezo minne iliyopita ya ligi ya Morocco licha ya kuwa uongozi ulikuwa ukimlipa pesa nzuri,mahitaji yote ya msingi ikiwemo msaada wa kiufundi.

    Toshack,67,alianza kukinoa kikosi cha Januari 2014 na katika msimu wake wa kwanza aliisaidia miamba hiyo ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Morocco maarufu kama Botola Pro.Msimu uliofuata alimaliza katika nafasi ya pili iliyoipa timu hiyo tiketi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa Afrika.

    Kabla ya kutua Wydad Casablanca,Toshack,aliwahi kuvifundisha vilabu vya Real Madrid,Real Sociedad,Swansea City pamoja na kuzinoa timu za taifa za Wales na Macedonia.Pia aliwahi kuichezea klabu ya Liverpool akiwa kama mshambuliaji.

    Wydad Casablanca pia imewafuta kazi waliokuwa makocha wake wa makipa Younes Koutaya na Driss Ouajou.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KOCHA WA REAL MADRID ATUPIWA VIRAGO MOROCCO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top