728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, September 15, 2016

    RONALDO AJA NA REKODI NYINGINE UEFA BAADA YA MESSI KUWEKA YA KWAKE


    Madrid,Hispania.

    MASAA 24 baada ya Staa wa Argentina,Lionel Messi,kuweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyefunga mabao matatu/hat-tricks nyingi zaidi katika historia ya michuano ya klabu bingwa Ulaya Jumanne usiku pale alipofunga mabao matatu na kuiwezesha Barcelona kuichapa Celtic mabao 7-0 huko Nou Camp,hasimu wake Mreno Cristiano Ronaldo nae kaweka rekodi nyingine kubwa.

    Bao la mpira wa adhabu (faulo/free kick) alilofunga dakika ya 88 dhidi ya klabu yake ya zamani ya Sporting Lisbon jana Jumatano Usiku katika mchezo wa kwanza wa kundi F wa klabu bingwa Ulaya limemfanya Ronaldo afikishe mabao 12 na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi ya mipira ya adhabu katika historia ya michuano hiyo.

    Mbali ya bao hilo kumweka Ronaldo,31,juu katika chati ya wafungaji mahiri wa mipira ya adhabu wa muda wote pia bao hilo limekuwa la 550 kuwahi kufungwa na mshindi huyo wa tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya.

    Ifuatayo ni orodha ya wachezaji waliofunga mabao mengi zaidi kwa mipira ya adhabu/faulo katika historia ya michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya.

    Cristiano Ronaldo - 12 

    Alessandro Del Piero – 11

    Juninho – 10 

    Rivaldo – 8 


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: RONALDO AJA NA REKODI NYINGINE UEFA BAADA YA MESSI KUWEKA YA KWAKE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top