Mtwara,Tanzania.
LIGI kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea tena kesho Jumatano kwa michezo mitatu kuchezwa katika miji ya Mtwara,Dar Es Salaam na Mbeya.
Huko Mtwara Ndanda FC watakuwa katika uwanja wao wa nyumbani wa Nangwanda Sijaona kuwakaribisha mabingwa watetezi wa ligi hiyo,Dar Young Africans.
Azam FC watakuwa katika dimba la Sokoine,Mbeya kuvaana na wenyeji wao Maafande wa Tanzania Prisons.
Mabingwa wa zamani wa ligi hiyo Simba SC watakuwa katika uwanja wa Uhuru (Shamba la Bibi) Dar Es Salaam kupimana ubavu na Maafande wa Ruvu Shooting Stars.Michezo yote itaanza saa 10:00 Jioni.
0 comments:
Post a Comment