728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, September 02, 2016

    KIRAFIKI:UFARANSA YAICHAPA ITALIA,URENO YAPIGA MTU MKONO (+VIDEO)

    Bari,Italia.

    Antony Martial (Pichani) akishangilia bao aliloifungia Ufaransa dakika ya 17 na kuiwezesha kuibuka na ushindi wa mabao 3-1ugenini dhidi ya Italia huko Bari,Italia.

    Mabao mengine ya Ufaransa yamefungwa na Olivier Giroud dakika ya 28' na Layvin Kurzawa dakika ya 81.Bao la wenyeji Italia limefungwa na Graziano Pellè dakika ya 21ya mchezo.

    Katika mchezo huo ambao Italia ilikuwa ikianza kunolewa kwa mara ya kwanza na kocha wake mpya Giampiero Ventura ilishuhudiwa kiungo Mpya wa Manchester United Paul Pogba akitamba vilivyo baada ya kutoa pasi mbili za mabao.

    Katika mchezo mwingine wa kirafiki Ubelgiji imechapwa mabao 2-0 na Hispania.Uholanzi ikiwa nyumbani Eindhoven imefungwa mabao 2-1 na Ugiriki.Ureno ikicheza bila ya nahodha wake Cristiano Ronaldo imeifanyia mauaji Gibraltar baada ya kuifunga mabao 5-0.

    Mabao ya Ureno yamefungwa na Luis Nani aliyefunga mara mbili,Joao
    Cancelo, Bernardo Silva na Pepe.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KIRAFIKI:UFARANSA YAICHAPA ITALIA,URENO YAPIGA MTU MKONO (+VIDEO) Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top