Quito,Ecuador.
HATIMAYE Brazil imepata ushindi wake wa kwanza ugenini nchini Ecuador tangu mwaka 1983 baada ya Alfajiri ya leo kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji wao huko Quito katika mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi.
Mabao ya Brazil yamefungwa na Neymar Jr kwa mkwaju wa penati dakika ya 72 huku mengine yakifungwa na kinda Gabriel Jesus dakika za 87 na 90.Huo ulikuwa ni mchezo wa kwanza kwa Jesus akiwa na kikosi cha wakubwa cha Brazil.
Katika mchezo huo Ecuador walilazimika kumaliza mchezo wakiwa pungufu baada ya beki wao Juan Carlos Paredes kulimwa kadi ya pili ya njano baada ya kumchezea madhambi Renato Augusto
Ushindi huo umeifanya Brazil kusogea hadi nafasi ya nne katika msimamo wa mbio za kufuzu Kombe la Dunia kutoka ukanda wa Amerika ya Kusini maarufu kama CONMEBOL.
0 comments:
Post a Comment