Stavanger,Norway.
JOEL Campbell (Pichani) amefunga mabao mawili na kuiongoza Arsenal kuichapa Viking FK ya Norway kwa jumla ya mabao 8-0 katika mchezo Wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa katikka uwanja wa Viking Stadium,Stavanger-Norway.
Mabao mengine ya Arsenal yamefungwa na Santi Cazorla,Theo Walcott,Alex Iwobi aliyefunga mara mbili Chuba Akpom na Michael Haukas aliyejifunga akiwa katika harakati za kuokoa hatari langoni mwake.Cazorla alikosa penati mwanzoni mwa mchezo.
Ushindi huo ni wa tatu kwa Arsenal katika michezo minne ya kirafiki ya kujipima nguvu.Arsenal itashuka tena dimbani wiki ijayo kucheza na Manchester City katika mchezo mwingine wa kirafiki.
Kikosi Kilichoshuka Dimbani Leo:
Arsenal: Ospina, Debuchy, Bielik, Gabriel,Gibbs,Coquelin, Elneny, Oxlade-Chamberlain,Cazorla,Campbell, Walcott.
Akiba: Cech, Martinez, Bellerin, Holding,Monreal, Zelalem, Reine-Adelaide, Iwobi,Willock, Akpom.
0 comments:
Post a Comment