728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, August 15, 2015

    DE GEA AUFUNGUKIA UONGOZI MANCHESTER UNITED

    Mlinda mlango wa Manchester United David De Gea ameuambia uongozi wa klabu yake kuwa ''hakutaka kucheza'' kabla ya kuachwa nje kwenye mchezo wa ufunguzi wa msimu mpya.
    Meneja Louis van Gaal hatamtumia mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania mwenye miaka 24 mpaka dirisha la usajili kufungwa huku kukiwa na uvumi wa kujiunga na Real Madrid.
    Mchezaji huyo bora wa Man U wa misimu miwili alimwambia kocha wa makipa Frans Hoek kuwa hakuwa tayari kwa asilimia 100.
    Mchezaji wa kimataifa wa Argentina Sergio Romero alianza katika mchezo huo walioshinda dhidi ya Tottenham. De Gea kwa mara nyingine ameachwa nje kwenye kikosi kilichovaana na Aston Villa jana ijumaa.
    ''Sifanyi maamuzi yote peke yangu,'' alisema Van Gaal.''Nina waalimu wawili wasaidizi pamoja na kocha wa makipa Frans Hoek. ''Fans alikua na mazungumzo na De Gea na amekubaliana na kila kitu kuhusu maamuzi yetu''
    Van Gaal amesema kuwa yeye pamoja na benchi zima la ufundi walimtanzama De Gea kwenye mazoezi na kugundua kuwa mchezaji huyo wa zamani wa Atletico Madrid ''siyo yule wa siku zote''
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: DE GEA AUFUNGUKIA UONGOZI MANCHESTER UNITED Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top