London,England.
Klabu ya Arsenal imeibuka na ushindi wa kwanza wa ligi kuu England baada ya leo kuibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya klabu ngumu ya Crystal Palace katika mchezo wa mapema uliopigwa katika dimba la Selhurst Park, jijini London.
Arsenal ilipata bao lake la kwanza dakika ya (16) kupitia kwa straika wake Mfaransa Olivier Giroud aliyefunga kwa "Tiki Taka" akiunganisha vyema krosi ya kiungo Mesut Ozil baada ya bao hilo Crystal Palace iliamka na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha lililofungwa na mlinzi Joel Ward dakika ya (28) ya mchezo.
0 comments:
Post a Comment