Paul Manjale, Dar Es Salaam.
WEKUNDU wa Msimbazi,Simba SC wameendelea kukonga nyoyo za mashabiki wao katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya joto baada ya leo mchana kumsajili beki wa zamani wa Mtibwa Sugar,Ally Shomary.
Shomary mwenye uwezo wa kucheza nafasi nyingi uwanjani amejiunga na Simba SC kwa mkataba wa miaka miwili baada ya kumaliza mkataba wake na Mtibwa Sugar ya Manungu,Morogoro.
Shomary anakuwa mchezaji wa sita kujiunga na Simba SC tangu kumalizika kwa ligi Kuu ya soka ya Vodacom Tanzania Bara maarufu kama VPL.
Wengine ni mlinda mlango Emanuel Elias Mseja aliyetokea Mbao FC,Jamal Mwambeleko aliyesajiliwa kutoka Mbao FC, Yussuf Mlipili kutoka Toto Africans.Shomary Kapombe na John Bocco Adebayor wote kutoka Azam FC.
0 comments:
Post a Comment