728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, June 15, 2017

    KASEPA:Mbrazil aliyeipa Gor Mahia ubingwa wa SportPesa Cup abwaga manyanga.

    Ze Maria (Kulia)


    Nairobi,Kenya.

    IKIWA haijapita hata wiki moja tangu aipe Gor Mahia ubingwa wake wa kwanza wa michuano mipya ya SportPesa Cup,Kocha Mbrazil Jose Marcelo Ferreira maarufu kama Ze Maria amebwaga manyanga kuifundisha timu hiyo.

    Katika barua yake aliyomwandikia Mwenyekiti wa timu hiyo,Ambrose Rachier,Ze Maria ameushukuru uongozi wa Gor Mahia kwa kumpa nafasi ya kuinoa timu hiyo lakini hakuweka wazi kilichomwondoa mapema kwenye timu hiyo inayoshika nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi kuu ya Kenya (KPL).

    Ze Maria mwenye umri wa miaka 43 alijiunga na Gor Mahia Machi mwaka jana kuchukua nafasi ya kocha Mscotland,Frank Nuttall .

    Katika msimu wake wa kwanza, Ze Maria aliiongoza Gor Mahia kushika nafasi ya pili kabla ya mwaka huu kuiacha ikiwa nafasi ya kwanza baada ya kujikusanyia pointi 27 mpaka sasa.

    Ze Maria mwenye uwezo wa kuzungumza lugha nne za Kireno,Kiingereza,Kiitaliano na Kihispania alianza kazi ya ukocha mwaka 2010 na kufanikiwa kuhudumu katika mataifa ya Romania na Saudia Arabia.

    Kabla ya hapo Ze Maria aliwahi kucheza soka kwa mafanikio katika nchi za Hispania na Italia ambapo alitamba na Inter Milan akicheza kama mlinzi wa kulia.

    Aidha Ze Maria alifanikiwa kuichezea timu ya taifa ya Brazil michezo 46.Pia aliiwezesha timu hiyo kutwaa medali ya fedha kwenye michuano ya Olimpiki ya mwaka 1996 iliyofanyika Atlanta,Marekani kabla ya mwaka mmoja baadae kuwa sehemu ya kikosi cha Brazil kilichotwaa kombe la mabara nchini Ufaransa.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KASEPA:Mbrazil aliyeipa Gor Mahia ubingwa wa SportPesa Cup abwaga manyanga. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top