728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, June 01, 2017

    USAJILI:Klaas-Jan Huntelaar arejea Ajax


    Amsterdam, Uholanzi.

    AJAX imemsajili kwa mara nyingine mshambuliaji wake wa zamani Mholanzi,Klaas-Jan Huntelaar baada ya kumaliza mkataba wake FC Schalke 04 ya Ujerumani.

    Huntelaar mwenye umri wa miaka 33 amesaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuichezea klabu hiyo aliyoihama miaka minane iliyopita.


    Huntelaar alijiunga na Ajax kwa mara ya kwanza Januari 2006 kabla ya kutimka mwaka 2009 na kukiunga na Real Madrid ya Hispania. Akiwa na Ajax Huntelaar alifanikiwa kufunga mabao 105 katika michezo 137.

    Ajax imemsajili Huntelaar ili kuiongezea makali kikosi chake ambacho hakijatwaa ubingwa wa Eredivisie tangu mwaka 2014.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: USAJILI:Klaas-Jan Huntelaar arejea Ajax Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top