728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, June 01, 2017

    Manchester United yaachana na Antoine Griezmann

    Manchester, England.

    MABINGWA wa Europa ligi, Manchester United wameachana na mpango wa kutaka kumsajili mshambuliaji mahiri wa Atletico Madrid,Antoine Griezmann.

    Uwamuzi huo ambao umewashitua wengi umetangazwa muda mfupi uliopita baada ya taarifa kuibuka kuwa rufaa ya Atletico Madrid iliyokuwa ikisikilizwa kwenye mahakama ya michezo ya FIFA (CAS) imetupiliwa mbali na badala yake klabu hiyo ya Vicente Cardeloni itaendelea kuitumikia adhabu yake ya kuzuiwa kusajili kwa kipindi cha madirisha mawili ya usajili.

    Mapema mwaka huu Atletico Madrid na wapinzani wao Real Madrid walifungiwa kufanya usajili baada ya kukutwa na hatua ya kufanya udanganyifu kwenye usajili wa wachezaji wenye umri mdogo.

    Manchester United imeamua kujiweka pembeni baada ya kugundua kuwa Atletico Madrid haitaweza kumwachia Griezmann kirahisi licha ya hukumu hiyo ya FIFA kutoizuia klabu hiyo kuuza wachezaji.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Manchester United yaachana na Antoine Griezmann Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top