Stoke, England.
KIUNGO wa zamani wa Manchester United,Darren Fletcher leo amejiunga na Stoke City akitokea West Bromwich Albion.
Fletcher mwenye umri wa miaka 33 amejiunga na Stoke City kwa mkataba wa miaka miwili kwa uhamisho huru baada ya kumaliza mkataba wake klabuni West Bromwich Albion.
Fletcher alijiunga na West Bromwich Albion mwaka 2015 akitokea Manchester United baada ya Kocha mkuu wa wakati huo Mholanzi, Louis Van Gaal kutomuhitaji kikosini kwake.
Msimu uliopita Fletcher aliichezea West Bromwich Albion michezo yote 38 ya ligi kuu England akifunga mabao mawili na kutengeneza mengine matatu.
0 comments:
Post a Comment