Geneva,Uswisi.
SHIRIKISHO la soka duniani (FIFA) leo Alhamisi ya Juni,01 limetoa orodha mpya ya viwango vya ubora wa mchezo huo kwa nchi wanachama.
Katika orodha hiyo Tanzania imeshuka kwa nafasi nne kutoka nafasi ya 135 mwezi Aprili mpaka nafasi ya 139 kwa mwezi Mei ambao umeisha jana Jumatano.
Kwa Afrika Mashariki,Uganda iko nafasi ya kwanza,kidunia nafasi ya 71 ikifuatiwa na Kenya (74),Rwanda (128), Tanzania (139) na Burundi (148).
Nafasi ya kwanza duniani bado imeendelea kushikiliwa na Brazil ikifuatiwa na Argentina, Ujerumani,Chile,Colombia,Ufaransa,Ubelgiji,Ureno,Uswisi,Hispania na Poland.
Kwa Afrika,Misri bado iko kileleni,kidunia iko nafasi ya 20 ikifuatia na Senegal (27), Cameroon (32),Nigeria (38),Congo DR (39) na Ivory Coast (47).
Nchi za Somalia na Tonga zimeshika mkia.Zimeshika nafasi ya 206.Orodha nyingine itatoka Alhamisi ya Julai 06 mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment