728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, June 14, 2017

    Benni McCarthy kocha mkuu mpya Cape Town City


    Cape Town, Afrika Kusini.

    MSHAMBULIAJI nyota wa zamani wa Bafana Bafana, Benni McCarthy (Kulia) ameteuliwa kuwa kocha mkuu mpya wa klabu ya Cape Town City inayoshiriki ligi kuu nchini Afrika Kusini.

    McCarthy mwenye umri wa miaka 40 sasa amejiunga na Cape Town City kwa mkataba wa miaka mitatu kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Eric Tinkler aliyejiunga na klabu ya SuperSport United. 

    Tinkler ameiacha Cape Town City baada ya msimu uliopita kuiongoza kumaliza ligi ikiwa katika nafasi ya tatu huku pia akiiongoza klabu hiyo kutwaa kombe la mtoano la Telkom.

    Kabla ya kupewa kibarua cha kuinoa Cape Town City,McCarthy alikuwa akifanya kazi ya uchambuzi katika kituo cha luninga cha Super Sports.Pia aliwahi kuwa kocha msaidizi katika klabu ya St. Truiden ya nchini Ubelgiji.Kibarua cha kuinoa Cape Town City ni kibarua chake cha kwanza akiwa kama kocha mkuu.

    Ikumbukwe kabla ya kugeukia ukocha McCarthy aliwahi kutamba katika vilabu vya Ajax Amsterdam ya Uholanzi,FC Porto ya Ureno aliyoisaidia kutwaa taji la klabu bingwa Ulaya,Celto Vigo na Hispania pamoja na vilabu vya England vya Blackburn Rovers na West Ham.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Benni McCarthy kocha mkuu mpya Cape Town City Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top