Dar Es Salaam,Tanzania.
VIJANA wanne waliochini ya umri wa miaka 17 (U-17) waliochaguliwa kwenye majaribio ya wazi ya Wilaya ya Kinondoni, yaliyofanyika Uwanja wa Tanganyika Packers juzi Jumamosi yamehitimisha majaribio kwa upande wa mkoa wa Dar es Salaam.
Azam FC inayoendesha zoezi hilo la kusaka wachezaji wa kuunda timu bora ya vijana wa umri huo,imefanikiwa kuvuna vijana 15 bora kwa mkoa wa Dar es Salaam huku ikiwafanyia majaribio jumla ya vijana 1083 katika maeneo matatu waliyozunguka ndani ya jiji hili.
Mtaalamu wa Maendeleo ya Soka la Vijana Azam FC, Tom Legg,anayeshirikiana na kocha John Matambala kwenye zoezi hilo,walifanikiwa kuvuna vijana watano kati ya 423 kwenye Wilaya ya Temeke na Kigamboni kabla ya kupata sita (448) ndani ya Wilaya ya Ilala.
Wakati wakihitimisha zoezi la mwisho jijini Dar es Salaam jana, jopo hilo liliwafanyia majaribio vijana 212 kutoka Kinondoni na kuridhishwa na wanne bora pekee.
Baada ya zoezi hilo kuhitimika Dar es Salaam, hivi sasa litaamia maeneo mengine mikoani kuhusu taarifa ya wapi tunakoelekea, tutawajuza hivi karibumi juu ya mahali na muda.
0 comments:
Post a Comment