Kampala,Uganda.
UGANDA imepania kuvunja mwiko wa kutofuzu michuano ya AFCON kwa takribani miaka 39 pale Jumapili jioni itakaposhuka katika uwanja wake wa nyumbani wa Mandela Namboole Stadium jijini Kampala,kuvaana na Comoro katika mchezo wao wa mwisho wa kundi D wa kuwania tiketi michuano ya Afrika mwakani nchini Gabon.
Katika mchezo huo unaotarajiwa kuhudhuriwa na watazamaji zaidi ya 42,000 Uganda inaingia uwanjani ikihitaji ushindi wowote ule dhidi ya Comoro ili iweze kufuzu fainali za AFCON kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1978.
Uganda iko nafasi ya pili katika msimamo wa kundi D ikiwa na pointi 10 sawa na vinara Burkina Faso wenye pointi 10 pia ambao nao wanahitimisha safari yao kwa kuvaana na Botswana.
Wakati huohuo taarifa kutoka nchini Uganda zinasema wachezaji wote wa kikosi cha Uganda Cranes pamoja na benchi zima la ufundi la timu hiyo kila mmoja ameahidiwa kitita cha Dola 10,000 kama zawadi ikiwa wataifunga Comoro na kufuzu AFCON.
0 comments:
Post a Comment