Nelspruit,Afrika Kusini.
RASMI timu ya taifa ya Afrika Kusini maarufu kama Bafana Bafana imetupwa nje ya michuano ya kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya AFCON mwakani nchini Gabon baada ya Ijumaa usiku ikiwa nyumbani kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Mauritania katika mchezo wa mwisho wa kundi M uliochezwa katika uwanja wa Mbombela Stadium huko Nelspruit.
Wageni Mauritania ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza baada ya Dialo Guideye kufunga katika dakika ya 17 ya mchezo.Bao hilo halikudumu sana kwani dakika ya 26 Hlompho Kekana aliwasawazishia bao wenyeji Bafana Bafana baada ya kufyatua mkwaju Mkali.
Katika mchezo huo Mauritania walilazimika kumaliza wakiwa pungufu baada ya mlinzi wake Ismael Diakhite kuonyeshwa kadi ya pili ya njano dakika ya 75 kwa mchezo mbaya.
Aidha katika mchezo huo Thulani Hlatshwayo aliinyima ushindi Bafana Bafana baada ya mkwaju wake wa penati wa dakika ya 85 kushindwa kulenga lango na kwenda nje.
Matokeo hayo yameiacha Cameroon peke yake kutoka kundi M ikikata tiketi ya kucheza michuano ya AFCON mwakani nchini Gabon.
VIKOSI
Afrika Kusini: Khune; Mobara, Mphahlele,Hlatshwayo, Langerman - Jali, Kekana (Furman 67'), Makola, Modiba - Vilakazi (Motupa 83'), Gabuza (Rantie 60')
Mauritania: Souleymane (Boubacar 46'); Wade,N'Diaye, Sally, Camara - Guideye (Gueye 72'),Yaly, El Id (Denna 64') - Khalil, Bagili, Diakhite
0 comments:
Post a Comment