London,Uingereza.
MENEJA wa Arsenal,Arsene Wenger,jana Ijumaa usiku ametangaza kikosi cha nyota 25 kitakachoiwakilisha klabu hiyo katika michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya maarufu kama UEFA Champions League.
Kama ilivyotarajiwa nyota wapya wa klabu hiyo Rob Holding, Shkodran Mustafi,Granit Xhaka na Lucas Perez wamejumuishwa katika kikosi hicho pamoja na wenyeji Yaya Sanogo, Carl Jenkinson na Mathieu Debuchy.
Granit Xhaka
Aidha katika kikosi hicho Wenger amelazimika kutowajumuisha nyota wake wawili Danny Welbeck na Per Mertesacker kutokana na kuwa nje ya dimba wakiuguza majeraha mbalimbali ambayo yatawaweka nje mpaka kipindi cha msimu wa krismasi.
Kikosi Kamili kiko kama ifuatavyo:
Makipa:David Ospina, Emiliano Martinez, Petr Cech
Mabeki:Mathieu Debuchy, Gabriel,Laurent Koscielny, Rob Holding, Nacho Monreal, Shkodran Mustafi, Carl Jenkinson, Kieran Gibbs
Viungo:Aaron Ramsey, Mesut Ozil,Santi Cazorla, Granit Xhaka, Jeff Reine-
Adelaide, Francis Coquelin, Mohamed Elneny, Krystian Bielik
Washambuliaji:Alexis Sánchez, Lucas, Olivier Giroud, Theo Walcott, Alex Oxlade-Chamberlain, Yaya Sanogo
Arsenal imepangwa kundi A pamoja na vilabu vya Paris Saint-Germain, Basel na Ludogorets Razgrad.Itaanza kibarua chake ugenini Septemba 13 kwa kuvaana na Paris Saint-Germain.
Ratiba:
PSG vs Arsenal (13 Septemba)
Arsenal vs FC Basel (28 Septemba)
Arsenal vs Ludogorets (19 Octoba)
Ludogorets vs Arsenal (1 Novemba)
Arsenal vs PSG (23 Novemba)
FC Basel vs Arsenal (6 Decemba)
0 comments:
Post a Comment