728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, September 02, 2016

    SERGIO AGUERO AFUNGIWA MICHEZO MITATU


    London, Uingereza.

    CHAMA cha soka cha England (FA) kimetangaza kumfungia michezo mitatu Mshambuliaji wa Manchester City,Sergio Aguero,baada ya kuitupa rufaa yake.

    Aguero amekumbana na adhabu hiyo kali baada ya kukutwa na hatia ya kumchapa kiwiko usoni beki wa West Ham,Winston Reid,Agosti 28 katika mchezo ambao Manchester City ikiwa nyumbani Etihad Stadium ilishinda kwa mabao 3-1.

    Aguero alinusurika kutolewa uwanjani dakika ya 78 baada ya mwamuzi Andre Marriner kushindwa kuliona tukio hilo.Lakini FA iliamua kulivalia njuga tukio hilo na kulifikisha katika kamati yake ya maadili ambayo baada ya kupitia ripoti mbalimbali imemkuta akiwa na hatia mshambuliaji huyo mfupi.

    Michezo ambayo Aguero ataikosa ni ule wa ligi kuu wa Septemba 10 dhidi ya Manchester United,Bournemouth na mchezo wa kombe la ligi (EFL) dhidi ya Swansea City.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SERGIO AGUERO AFUNGIWA MICHEZO MITATU Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top