INTER MILAN imetoka nyuma na kuibamiza Juventus kwa mabao 2-1 katika mchezo mkali wa ligi ya Seria A uliochezwa Jumapili Usiku katika uwanja wa San Siro uliopo jijini Milan.
Stephan Lichsteiner alianza kuwafungia wageni Juventus bao la kuongoza dakika ya 66 kwa kichwa lakini bao hilo halikudumu sana kwani dakika mbili baadae yaani dakika ya 68 ,Mauro Icardi,aliifungia Inter Milan bao la kusawazisha kwa kichwa likiwa ni bao lake la saba dhidi ya Juventus katika michezo minane iliyopita.
Mchezo ukiwa umebakiza dakika 12 kwisha mtokea benchi,Ivan Perisic,aliifungia Inter Milan bao la ushindi kwa kichwa akiunganisha krosi safi ya nahodha Mauro Icardi na kuipa Inter Milan ushindi wa kwanza dhidi ya Juventus tangu mwaka 2012.
Aidha katika mchezo huo Inter Milan ililazimika kumaliwa ikiwa pungufu baada ya kiungo wake Ever Banega kulimwa kadi nyekundu dakika ya 90 kwa mchezo mbaya.
Ushindi huo umeifanya Inter Milan ipande mpaka nafasi ya sita baada ya kufikisha pointi saba,Juventus imeshuka mpaka nafasi ya pili ikibaki na pointi zake nane nyuma ya vinara Napoli wenye pointi tisa.
0 comments:
Post a Comment