728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, September 17, 2016

    MTANZANIA JUMA LIUZIO NA ZESCO YAKE KIBARUANI LEO JIONI NUSU FAINALI YA LIGI YA MABINGWA AFRIKA


    Ndola,Zambia.

    KLABU ya Zesco United ya Zambia inayochezewa na Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania,Juma Ndanda Luizio,jioni ya leo itajitupa katika uwanja wake wa nyumbani wa Levy Mwanawasa katika mji wa Ndola kuvaana na klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini katika mchezo wa kwanza wa hatua ya nusu fainali ya klabu bingwa Afrika.

    Hii ni mara ya kwanza katika historia kwa vilabu vya Zambia na Afrika Kusini kukutana katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Afrika.Kabla ya hapo ziliwahi kukutana katika hatua za awali pekee yake.

    Pia ni mafanikio kwa klabu ya Zesco United kwani imekuwa ni timu ya kwanza kutoka nchini Zambia kuwahi kufika katika hatua ya nusu fainali ya klabu bingwa Afrika.

    Zesco United inaingia katika mchezo wa leo ikiwa na rekodi ya kutopoteza mchezo wowote wa michuano ya Afrika katika uwanja wake wa nyumbani tangu mwaka 2008.

    Kocha wa Zesco United,George Lwandamina,atakuwa akiwategemea washambuliaji wake Jesse Were,Idris Mbombo na Juma Liuzio kupata ushindi dhidi ya Mamelodi Sundowns lakini atazikosa huduma za kiungo wake mchezeshaji Cletus Chama ambaye amefungiwa kucheza mchezo wa leo na ujao.

    Baada ya mchezo wa leo timu hizo zitarudiana tena katika mchezo wa mkondo wa pili utakaochezwa Jumamosi,Septemba 24 mwaka huu Atteridgeville huko Johannesburg Afrika Kusini.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MTANZANIA JUMA LIUZIO NA ZESCO YAKE KIBARUANI LEO JIONI NUSU FAINALI YA LIGI YA MABINGWA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top