Madrid,Hispania.
STAA wa Real Madrid Mreno Cristiano Ronaldo anajiandaa kuweka rekodi nyingine hivi karibuni hii ni baada ya kuripotiwa kuwa karibu kumfikia Staa wa kike wa Marekani Taylor Swift kwa kuwa na wafuasi wengi zaidi katika mitandao ya kijamii.
Kwa mujibu wa taasisi ya Madrid agency Apple Tree Communications,mpaka sasa Ronaldo,amefikisha jumla ya wafuasi Milioni 238 katika mitandao yake ya kijamii ya Facebook,Twitter na Instagram.Idadi ambayo inazidiwa pekee na mwimbaji wa Marekani Taylor Swift mwenye wafuasi Milioni 246.
Hii ina maana kwamba sasa Ronaldo anahitaji wafuasi milioni 8 na ushee ili aweze kuwa mtu mwenye wafuasi wengi zaidi duniani kitu ambacho kimo ndani ya uwezo wake kwani katika kipindi cha siku 30 zilizopita Ronaldo amefanikiwa kujiongezea wafuasi Milioni 5.4 dunia kote.
Hayo ni mafanikio mengine kwa Ronaldo kwani mwezi Februari mwaka huu aliweka rekodi ya kuwa mwanamichezo wa kwanza duniani kuvuka idadi ya kuwa na wafuasi milioni 200 wanaomfuatilia katika mitandao ya kijamii.
Rekodi ambayo ilimfanya awe mbele ya hasimu wake,nyota wa Barcelona Lionel Messi pamoja na nyota wa Basketball LeBron James,Michael Jordan, Kobe Bryant, Kevin Durant na Steph Curry.
Waimbaji Katy Perry, Selena Gomez na Rihanna wametipotiwa kumfuatia Ronaldo wakiwa na wafuasi Milioni 219,Milioni 205 na Milioni 190.
Tafiti zinaonyesha kuwa watu wanaoongoza kuwa na ushawishi/mvuto mkubwa katika mitandao ya kijamii duniani ni mastaa wa kike wa Marekani ambapo 13 kati ya 20 wanaoongoza kuwa na wafuasi wengi ni duniani ni wanamuziki.Asilimia 60 ni wanawake na asilimia 65 ni Wamarekani.
0 comments:
Post a Comment