Dar Es Salaam,Tanzania.
MCHEZO wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliokuwa uchezwe Jumamosi ya Septemba 17 katika dimba la Uwanja wa Taifa,Dar Es Salaam kati ya Simba SC na Azam FC umesogezwa mbele mpaka Jumatano ya Septemba 21,2016.
Sababu za kuahirishwa kwa mchezo huo ni kuwa siku hiyo ya Jumamosi uwanja huo utakuwa ukitumiwa na timu ya taifa ya vijana ya Congo Brazzaville U-17 kwa ajili ya mazoezi yake ya kujiandaa na mchezo wake wa Jumapili wa kuwania kufuzu michuano ya Afrika ya vijana dhidi ya wenyeji wao timu ya taifa ya vijana ya Tanzania,Serengeti Boys.
Ikumbukwe kanuni za mchezo wa mpira wa miguu za kimataifa zinaagiza nchi mwenyeji kuachia uwanja siku moja au saa 24 kabla ya mchezo wa ushindani.
0 comments:
Post a Comment