Dar Es Salaam,Tanzania.
LIGI KUU ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) imeendelea tena leo kwa mchezo mmoja wa ligi hiyo kuchezwa katika uwanja wa Uhuru,Dar Es Salaam ambapo wenyeji wa mchezo huo African Lyon wamechomoza na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mbao FC ya Mwanza.
Katika mchezo huo uliohudhuriwa na watazamaji wachache sana ilishuhudiwa Mbao FC ikiwa ya kwanza kupata bao la kuongoza kupitia kwa F Msiba dakika ya 28.
Kuingia kwa bao hilo kuliiamsha African Lyon ambayo ilikuja juu na kufanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 45 kupitia kwa Hood Mayanja.
Dakika ya 58 Hood Mayanja alikuwa shujaa tena kwa upande wa African Lyon baada ya kufunga bao la pili.Bao la tatu limefungwa na Tito Okello dakika ya 68 na kufanya mchezo uishe kwa African Lyon kushinda kwa mabao 3-1.
0 comments:
Post a Comment