Sunderland,England.
MASHAMBULIAJI Romelu Lukaku (Pichani) amefunga mabao matatu (hat trick) ndani ya dakika 11 na kuhitimisha ukame wa kucheza michezo 11ya ligi kuu England bila ya kufunga bao na kuisaidia klabu yake ya Everton kuichapa Sunderland mabao 3-0 Jumatatu usiku huko Stadium of Light,Sunderland.
Lukaku amefunga mabao hayo dakika za 60,68 na 71 na kuipaisha Everton mpaka nafasi ya tatu katika jedwali la msimamo wa ligi kuu ya England baada ya kufikisha alama 10 sawa na Chelsea iliyoko katika nafasi ya pili kutokana na kuwa na uwiano mzuri wa mabao.Manchester United imeshuka mpaka nafasi ya nne ikiwa na alama zake 9.
Matokeo hayo yameifanya Sunderland kushuka mpaka nafasi ya 19 baada ya kuambulia alama moja mpaka sasa licha ya kushuka dimbani mara nne.
0 comments:
Post a Comment