Bethlehem,Afrika Kusini.
KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa amevunja mkataba na iliyokuwa klabu yake ya zamani ya Free State Stars ( Ea Lla Koto) inayoshiriki ligi kuu ya Afrika Kusini maarufu ABSA Premiership.
Ngassa,27, ameripotiwa kuvunja mkataba huo kwa madai kuwa Free State Stars haina malengo ya kushinda taji.Napenda kushinda mataji.Nimezoea kushinda mataji.
Ngassa alijiunga na Free State Stars Mei 2015 kwa kandarasi ya miaka minne kwa ada ya R1.7m na kuweka rekodi ya kuwa mmoja kati ya wachezaji ghali zaidi wa klabu hiyo yenye makao yake makuu Bethlehem.
Wakati Ngassa akitimka,Free State Stars imeingia mkataba wa miaka mitatu na winga wa zamani wa Akademi ya FC Barcelona Mcameroon,Armand Ken Ella mitatu pamoja na Mganda Hamis Kiiza aliyesaini mkataba wa mwaka mmoja.
0 comments:
Post a Comment