MABINGWA watetezi wa ligi kuu ya England,Leceister City,wameanza vyema safari yao mpya ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya baada ya usiku huu kuichapa Club Brugge ya Ubelgiji kwa mabao 3-0 katika mchezo wa raundi ya kwanza wa kundi G uliochezwa katika uwanja wa Jan Breydel Stadium huko Brussels.
Marc Albrighton ndiye aliyekuwa shujaa wa Leceister City usiku huu baada ya kuifungia klabu hiyo bao lake la kwanza katika michuano hiyo.Mabao mengine ya Leceister City yamefungwa na Riyad Mahrez kwa mikwaju ya faulo na penati
Matokeo mengine ya kundi hilo,Porto ikiwa nyumbani Ureno imekwenda suluhu ya kufungana bao 1-1 na Copenhagen ya Denmark..
0 comments:
Post a Comment