728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, September 15, 2016

    RONALDO,MORATA WAIPA REAL MADRID USHINDI ULAYA (+VIDEO)


    Madrid,Hispania.

    REAL MADRID wameanza vyema kampeni za kuutetea ubingwa wa Ulaya walioutwaa msimu uliopita baada ya usiku huu kutoka nyuma na kuichapa Sporting Lisbon ya Ureno mabao 2-1 katika mchezo mkali wa kundi E uliochezwa katika uwanja wa Santiago Bernabeu.

    Wageni Sporting Lisbon ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza dakika ya 47 ya kipindi cha pili kupitia kwa Bruno Cesar.

    Kuingia kwa bao hilo kuliwaamsha Real Madrid ambao walianza kulishambulia lango la Sporting Lisbon kama nyuki na kufanikiwa kusawazisha dakika ya 89 baada ya Cristiano Ronaldo kufunga kwa mpira wa faulo.

    Mpira ukiwa unaelekea kuisha Alvaro Morata aliihakikishia Real Madrid pointi tatu baada ya kufunga bao la ushindi katika dakika ya 95 ya mchezo na kufanya mchezo uishe kwa wenyeji kushinda kwa mabao 2-1.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: RONALDO,MORATA WAIPA REAL MADRID USHINDI ULAYA (+VIDEO) Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top