728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, September 14, 2016

    KOCHA YANGA ASHTUKIA MECHI ZA SHINYANGA


    Dar Es Salaam,Tanzania.

    MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu bara Yanga wamesema wanakwenda Shinyanga kwa tahadhari wakijua wazi kuwa lazima wapambane kupata ushindi katika uwanja wa ugenini kwenye mchezo ujao dhidi ya Mwadui FC utakaochezwa Jumamosi.

    Kocha wa Yanga, Hans-van-der-Pluijm amesema wanakwenda kwa tahadhari wakijua wazi kuwa viwanja vya mikoani sio vizuri hivyo ni lazima wawe na mbinu za kupata matokeo katika mechi zote watakazocheza huko.

    “Ni wazi kuwa viwanja vya mikoani vina shida kwa hiyo nitazungumza na wachezaji wangu ni mbinu gani ya kufanya kuhakikisha tunafanya vizuri katika mchezo ujao na mingine itakayofuata,” alisema.

    Yanga imecheza michezo miwili ya nyumbani dhidi ya African Sports na kushinda mabao 3-0 na dhidi ya Majimaji mabao 3-0 na kupata sare ya bila kufungana katika mchezo mmoja wa mkoani dhidi ya Ndanda FC.

    Timu hiyo itakuwa na michezo miwili ya Kanda ya Ziwa dhidi ya Mwadui Jumamosi na Stand United utachezwa kwenye Uwanja wa Kambarage Shinyanga Septemba 25 na kurudi katika Uwanja wa Taifa Oktoba Mosi kuchuana na Simba.

    Yanga inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi saba katika michezo mitatu,ikishinda miwili na sare moja,nyuma ya Simba inayoshika nafasi ya pili ikiwa na pointi 10 sawa na Azam FC inayoongoza kileleni kwa pointi hizo 10 kwa michezo minne.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KOCHA YANGA ASHTUKIA MECHI ZA SHINYANGA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top