London,Uingereza.
WINGA wa Chelsea,Eden Hazard,ametangazwa mshindi katika kinyang'anyiro cha kumsaka mchezaji bora wa mwezi Agosti wa ligi kuu England.
Hazard,24,ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwabwaga washindani wake wa karibu Curtis Davies wa Hull City,Raheem Sterling wa Manchester City na Antonio Valencia wa Manchester United.
Jumla Hazard amepata kura asilimia 41%,akifuatiwa na Valencia aliyepata kura asilimia 34%.
Ndani ya mwezi Agosti Hazard amefunga mabao mawili katika michezo mitatu huku pia akitoa pasi 150 zilizowafikia walengwa.
Wakati Hazard akiibuka kinara kwa upande wa wachezaji,Kocha wa Manchester United,Jose Mourinho,yeye ametangazwa kuwa Kocha bora wa mwezi Agosti mbele ya Pep Guardiola wa Manchester City ,Mike Phelan wa Hull City na Antonio Conte wa Chelsea.
0 comments:
Post a Comment