728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, September 06, 2016

    JAMANI MOMO SISSOKO ANAREJEA TENA LIGI KUU ENGLAND

    Liverpool,Uingereza

    KAMA siyo leo basi kesho.Ishu iko hivi kiungo wa zamani wa Liverpool,Mohammed Sissoko (MoMo) muda wowote kuanzia sasa huenda akarejea tena kukipiga ligi kuu England.

    Sissoko,31,ambaye kwa sasa ni mcheza huru ameripotiwa kuwa kwenye majaribio katika klabu ya West Bromwich Albion na ikiwa mambo yatakwenda vyema atasaini kandarasi ya kuitumikia klabu hiyo yenye makao yake katika dimba la The Hawthorns.

    Jumamosi iliyopita Sissoko aliichezea West Bromwich Albion kwa dakika 60 kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya klabu ya India ya Delhi Dynamos na kuonyesha kiwango kizuri kilichomvutia kocha Tony Pulis.

    Sissoko alijiunga na Liverpool mwaka 2005 akitokea Valencia kwa ada ya £5.6m.Mwaka 2007 alikuwa sehemu ya kikosi cha Liverpool kilichotwaa ubingwa wa kombe la FA kwa kuifunga Westham United katika fainali.




    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: JAMANI MOMO SISSOKO ANAREJEA TENA LIGI KUU ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top