Njeru,Uganda.
MICHUANO ya CECAFA kwa upande wa wanawake ilianza kutimua vumbi lake jana Jumapili huko Njeru,Uganda kwa michezo miwili ya kwanza ya kundi A kuchezwa katika uwanja wa FUFA Technical Center.
Katika mchezo wa mapema ilishuhudiwa Zanzibar ikionjeshwa joto la jiwe baada ya kufungwa mabao 10-1 na Burundi.
Burundi ilijipatia mabao yake kupitia kwa Djazilla Uwimeza (3),Sakina Saidi (2), Aziza Misigiyimana (1),Bukuru Joe’lle (1), Neilla Uwimana (1) na Maggy Mumezero (2).
Bao la kufutia machozi kwa Zanzibar lilifungwa kwa mkwaju wa penati na nahodha wake Abdallah Abdullahi Mwajuma.Kipa wa Zanzibar Amina
Mohamed Kitambi alitolewa nje kwa kadi nyekundu kwa mchezo mbaya.
Katika mchezo wa pili Uganda nayo ilikiona cha mtema kuni baada ya kuchapwa mabao 4-0 na Kenya.
Mabao ya washindi Kenya yamefungwa na Mary Kinuthia Wanjiku (1),Esse Mbeyu Akida (2) na Vivian Corazon (1).
Michuano hiyo itaendelea tena leo jumatatu kwa michezo mmoja wa kundi B kuchezwa ambapo Tanzania Bara itashuka dimbani saa 10:00 Jioni kupepetana na Rwanda.
Jumanne
Burundi v Kenya (8:00 Mchana)
Zanzibar v Uganda (10:00 Jioni)
0 comments:
Post a Comment