London,Uingereza.
Meneja wa Bournemouth,Muingereza Eddie Howe,39, ameanza kutajwa kuwa mrithi wa
meneja wa Arsenal,Mfaransa Arsene Wenger,ambaye mkataba wake unaisha mwishoni
mwa msimu huu.
Kwa mujibu wa Neil Ashton wa gazeti la The Sun la Uingereza ni kwamba
tayari jina la meneja huyo wa Bournemouth limeshatua kwenye meza za wakuu wa
Arsenal na tayari limeshaanzwa kujadiliwa.
Howe ambaye msimu uliopita alifanikiwa kuibakiza Bournemouth ligi kuu
ameripotiwa kuwa na mvuto mkubwa ndani ya bodi ya wakuu wa Arsenal kutokana na
falsafa zake pamoja na ufundishaji wake.
Howe mwenye rekodi ya kuichezea Bournemouth michezo 270 akiwa kama mlinzi wa
kutumainiwa wa klabu alistaafu kucheza soka mwaka 2007 kutokana na majeruhi.Howe
amejizolea sifa kemkem kwa kuweza kuipandisha klabu hiyo kutoka daraja na pili
mpaka ligi kuu.
Arsenal imeanza kumfukuzia Howe kama tahadhari ikiwa meneja wake wa sasa
Wenger,66,ataamua kutosaini mkataba mpya na kujiweka pembeni.Mpaka sasa Wenger
bado hajatoa tamko kama ataendelea kusalia Arsenal ama ataondoka mwishoni mwa
msimu huu pindi mkataba wake utakapokuwa umekwisha.
0 comments:
Post a Comment