Liverpool,Uingereza.
SADIO Mane ameishusha presha klabu yake ya Liverpool baada ya kurejea mazoezini Melwood na kuzima uvumi ulionea kuwa alipata majeraha wakati akiichezea Senegal katika mchezo wa AFCON dhidi ya Namibia wikendi iliyopita.
Mane mwenye umri wa miaka 23 juzi Jumapili alitolewa uwanjani katika mchezo ambao Senegal ilimaliza michezo yake ya kuwania tiketi ya AFCON kwa kuichapa Namibia kwa mabao 2-0 mjini Dakar.
Mane amesema kuwa kutoka kwake uwanja Jumapili hakukuhusiana na kuumia na amesisitiza kuwa yuko tayari kuungana na wachezaji wenzake wa Liverpool katika maandalizi ya mchezo wa Jumamosi hii dhidi ya mabingwa Leceister City.
"Niko fiti.Ni kweli niligongwa kidogo nyuma ya goti,lakini haikuwa kitu kikubwa.Ilikuwa kipindi cha kwanza lakini niliweza kuendelea na mchezo.
Niliongea na Kocha na kwa kuwa tulikuwa na wachezaji wapya kikosini alitaka kuwajaribu.Akanibadili hivyo kutoka kwangu hakukuwa kwa sababu ya kuumia.
0 comments:
Post a Comment