London,Uingereza.
CHELSEA kwa kupenda wachezaji wa Kibrazil inaongoza
aisee!!Kama ulidhani David Luiz ndiyo mchezaji wa mwisho mwenye uraia wa Brazil
kujiunga na Chelsea msimu huu basi umeumia.
Ishu iko hivi mara tu dirisha la usajili litakapofunguliwa
tena mwezi Januari,Kiungo wa Santos ,Thiago Maia,19,ana asilimia kubwa za kutua
Stamford Blidge.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail la leo Jumatano ni kwamba
Chelsea imeliweka juu kabisa jina la
Maia katika orodha ya nyota itakaowaongeza pindi dirisha la usajili la majira
ya baridi la mwezi Januari litakapofunguliwa.
Imeripotiwa tayari Paundi Milioni 15 zimeshaandaliwa kwa
ajili ya kuinasa saini ya kiungo huyo aliyeiwezesha Brazil kutwaa medali ya
dhahabu ya michuano ya Olimpiki iliyofikia tamati mwezi mwezi uliopita.
0 comments:
Post a Comment