728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, October 06, 2015

    KIIZA NDIYE BORA ZAIDI SIMBA KWA MWEZI SEPTEMBA


    Katika kuongeza morali na kuwazawadia wachezaji wanaofanya vizuri, Klabu ya Simba ilianzisha Tunzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi kuanzia mwezi wa Septemba 2015.
    Mshindi wa mwezi wa September, 2015 ni Hamis Kizza ambapo amepata kura 250 kati ya kura 411 zilizopigwa na mashabiki na wapenzi wa Simba na soka wa Tanzania kwa ujumla kupitia simu za mkononi ambao pia wamejiunga na huduma ya Simba News.
    Akikabidhiwa tunzo na kocha mkuu wa Simba Dylan Kerr, mshambuliaji wa kimataifa Hamis Kizza alisema “namshukuru sana Mungu kwa kuniwezesha kufanikiwa kuwa mchezaji wa Kwanza kabisa kuchukua tunzo ya mchezaji bora kwa mwaka 2015, napenda kuwaahidi wapenzi na mashabiki wangu katika mchezo wa soka kuwa sasa hii ndio itakuwa chachu yangu ya kufanya vizuri zaidi nikiwa na klabu yangu ya Simba”.

    Kocha Kerr alipata nafasi ya kuongea na wachezaji baada ya kugawa Tunzo na Tsh 500,000 kwa mchezaji bora ambapo alisema “Simba Nguvu Moja, wachezaji wangu huu ni wakati wa kutoa ushindani mkubwa sana kwenye mchezo wetu wa soka, viongozi wamekuja na wazo la kutoa mchezaji bora na kila mtu hapa anaouwezo wa kuwa mchezaji bora ni kwa kufanya mazoezi, nidhamu ya mchezo ukiwa uwanjani na hata nje ya uwanja na kujituma hapo unaweza kuwa mchezaji bora wa mwezi”.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KIIZA NDIYE BORA ZAIDI SIMBA KWA MWEZI SEPTEMBA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top