728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, June 05, 2017

    SportPesa Cup:AFC Leopards yaizima Singida United na kutinga nusu fainali


    Dar Es Salaam,Tanzania.

    AFC Leopards ya Kenya imekuwa timu ya kwanza kutinga nusu fainali ya michuano mipya ya SportPesa Super Cup baada ya mchana wa leo kuitupa nje Singida United kwa kuifunga kwa penati 5-4 baada ya sare ya bao 1-1 katika muda wa kawaida.

    Singida United ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza kupitia kwa kiungo wa kimataifa wa Zimbabwe,Thafwaza Kutinyu aliyefunga kwa kichwa katika dakika ya 10 ya kipindi cha kwanza.Bao hilo lilidumu mpaka mapumziko.

    Kipindi cha pili AFC Leopards walifanikiwa kuibana vyema Singida United na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha katika dakika ya 68 ya mchezo kupitia kwa Oburu na kufanya dakika 90 ziishe matokeo yakiwa sare ya bao 1-1 na kuamuriwa ipigwe mikwaju ya penati ili kumpata mshindi.

    AFC Leopards walifunga penati zao zote tano huku Singida United wakifunga penati nne na kukosa moja kupitia kwa beki wake wa kushoto Hassani Chuku.

    AFC Leopards itacheza nusu fainali na mshindi kati ya Yanga na Tusker FC


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SportPesa Cup:AFC Leopards yaizima Singida United na kutinga nusu fainali Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top