Mombasa,Kenya.
Mshambuliaji African Lyon, Fredy Cosmas 'Balotelli' amesaini mkataba wa miaka mitatu wenye thamani oilioni za Kenya na klabu ya Bandari inayoshiriki Ligi Kuu ya nchi hiyo.
Meneja wa mchezaji huyo Gakumba Patrick alisema wamekubali kusaini mkataba huo baada ya kuahidiwa dau zuri la uhamisho pamoja na mshahara mnono.
Gakumba alisema anatamani kuchukua wachezaji wengine nyota wa Tanzania na kuwatafutia timu nje, lakini kumekuwa na mazingira magumu kwa wachezaji kukubali suala hilo.
“Unajua nilikuwa namtafutia timu itakayompa nafasi ya kucheza kwahiyo wakati natafuta nikajikuta tumefikia sehemu nzuri kimaslahi kwahiyo na hata nafasi ya kucheza hivyo nikaona bora tulimalizane kwa sababu nina uhakika hapa atakuwa yupo sehemu salama,” alisema.
“Wachezaji wapo wengi natamani kwenda nchi mbalimbali za Afrika, lakini wengi walikuwa na mikataba na timu zao.
"Naamini nitafanya kazi nzuri na wachezaji wa Kitanzania,” alisema wakala huyo Mnyarwanda.
0 comments:
Post a Comment