Dar Es Salaam,Tanzania.
Azam FC imeendelea kuvuna wachezaji kanda ya ziwa hii ni baada ya leo Jumamosi kumsajili kiungo matata wa Mbao FC ya Mwanza,Salmin Hoza.
Hoza aliyejizolea sifa kemkem msimu uliopita kwa kuonyesha kiwango bora akiwa na Mbao FC amejiunga na Azam FC kwa mkataba Wa miaka miwili.
Hoza anakuwa amchezaji wa tatu kujiunga na Azam FC ndani ya wiki kutokea timu za kanda ya ziwa.Wengine ni Wazir Junior aliyejiunga aliyetokea Toto Africans ya Mwanza na Mbaraka Yusuf aliyetokea Kagera Sugar ya mkoani Kagera.Wote wamejiunga kwa mkataba wa miaka miwili.
0 comments:
Post a Comment