Mosco,Urusi.
MABINGWA wa kombe la FA nchini England,Arsenal wameripotiwa kuwa mbioni kukubali kutoa kitita cha £10m ili kumsajili staa wa CSKA Moscow ya Urusi,Aleksandr Golovin.
Matandao wa habari za michezo wa nchini Urusi wa Sports.ru umedai kuwa umepata taarifa kutoka chanzo kimoja kilicho karibu na klabu ya CSKA Moscow kuwa Arsenal iko katika hatua za mwisho mwisho kumnasa staa huyo mwenye miaka 21.
Mtandao huo pia umeripoti kuwa baada ya kukamilika kwa usajili huo,CSKA Moscow itaomba kubaki na Golovin kwa mkopo wa msimu mmoja.
Msimu uliopita Golovin anayetajwa kuwa na kipaji kikubwa na mwenye uwezo wa kucheza namba 11,10 na namba 8 aliichezea CSKA Moscow michezo 37 akifunga mabao matatu na kupika mengine manne.
0 comments:
Post a Comment