Uyo,Nigeria.
NIGERIA wameonyesha kwamba kuwa na wachezaji wengi wanaocheza soka la kulipwa barani Ulaya inaweza ikawa siyo tija sana wakati mwingine hii ni baada Jumamosi usiku wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Godswill Akpabio kukubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Afrika Kusini (Bafana Bafana) ambayo sehemu kubwa ya wachezaji wake wanacheza soka nyumbani.
Mabao yaliyoipa ushindi huo Afrika Kusini ambao ni wa kwanza dhidi ya Nigeria kwenye mashindano rasmi yamefungwa na Tokelo Rantie kwa kichwa katika dakika ya 55.Bao la pili limefungwa na Percy Tau katika dakika ya 82.
Ushindi huo umeifanya Afrika Kusini ikae kileleni mwa msimamo wa kundi E baada ya kujikusanyia pointi tatu.
Vikosi
Nigeria: Akpeyi; Shehu,Awaziem, Ekong,Elderson; Onazi, Ndidi, Etebo; Simon, Iwobi (Musa 60'), Iheanacho.
Bafana: Khune, Mphahlele, Langerman,Mathoho, Hlatshwayo (c), Furman, Zungu,Zwane, Dolly, Vilakazi (Manyama 64'), Rantie (Tau 80')
0 comments:
Post a Comment