Basel,Uswisi.
MABINGWA wa Ulaya,Ureno,wamezianza vibaya mbio za kuisaka tiketi ya kombe la dunia la mwaka 2018 nchini Urusi baada ya usiku huu kuchapwa mabao 2-0 na Uswisi katika mchezo wa kwanza wa kundi B uliochezwa katika uwanja wa St.Jacob Park,Basel.
Mabao yote mawili ya washindi Uswisi yamefungwa katika kipindi cha kwanza cha mchezo kupitia kwa Breel Embolo dakika ya 23 na Admir Mehmedi dakika ya 30.
Aidha katika mchezo huo Uswisi ililazimika kumaliza ikiwa pungufu baada ya kiungo wake Granit Xhaka anayechezea Arsenal kutolewa nje ya dimba kufuatia kuonyeshwa kadi mbili za njano kwa mchezo mbaya.
0 comments:
Post a Comment