Dar Es Salaam,Tanzania.
YANGA SC imeionyesha Simba SC kuwa ukubwa siku zote ni dawa hii ni baada ya leo kuizidi ujanja na kumsajili kiungo wa Mbao FC,Pius Buswita kwa mkataba wa miaka miwili.
Usajili wa Buswita umekuja kama pigo kwa Simba SC ambao mapema wiki hii walisemekana kuwa walishamalizana na mchezaji huyo mwenye uwezo wa kucheza nafasi nyingi uwanjani ikiwemo winga na ushambuliaji.
Buswita anakuwa mchezaji wa pili kujiunga na Yanga SC baada ya mlinzi wa Jang'ombe Boys,Abdallah Hajji Shaibu maarufu kama Ninja ambaye nae ameingia mkataba wa miaka miwili.
0 comments:
Post a Comment