Dar Es Salaam,Tanzania.
JAMAL Malinzi amepata mpinzani wa kwanza kwenye mbio za kutetea kiti chake cha Urais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) baada ya leo Mwenyekiti wa zamani wa Yanga,Imani Madega (Pichani) kuchukua fomu ya kugombea wadhifa huo mkubwa kabisa duru za mpira wa miguu nchini.
Madega alifika kwenye ofisi za TFF zilizoko Karume jijini Dar Es Salaam asubuhi ya leo na kuchukua fomu tayari kuanza mawindo ya kumng'oa Malinzi madarakani.
Uchaguzi mkuu wa TFF umepangwa kufanyika Agosti 12 mwaka huu huko mkoani Dodoma.
0 comments:
Post a Comment