Lionel Messi
Madrid,Hispania.
STAA wa Barcelona na Argentina,Lionel Messi hawezi kupata namba kwenye kikosi cha sasa cha Real Madrid.Hii ni kwa mujibu wa kinda wa timu hiyo Marco Asensio.
Asensio mwenye umri wa miaka 21 ameungana na nahodha wake,Sergio Ramos kuutaka uongozi wa Real Madrid kutomwaga pesa kufanya usajili wowote wa nguvu katika kipindi hiki cha majira ya joto kwani tayari kikosi chao kiko nondo ile mbaya.
Marco Asensio (Kulia) akifanya vitu vyake uwanjani
Akijibu swali aliloulizwa na gazeti la Marca kama angependa kuona Messi akitua Real Madrid,bila kupepesa macho wala kuuma maneno,Asensio amesema kwasasa staa huyo kutoka Argentina hawezi kupata namba kwenye kikosi hicho kinachofundishwa na Zinedine Zidane.
Asensio anayekaribia kuingia mkataba mpya Real Madrid amesisitiza kuwa kama kikosi chao kitabaki kama kilivyo sasa bila kupanguka basi kitatisha zaidi msimu ujao.
0 comments:
Post a Comment