728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, June 15, 2017

    Manchester United yafungua usajili yamwaga noti za maana kwa beki wa Benfica


    Manchester,England.

    MABINGWA mara 20 wa ligi kuu ya soka nchini England,Manchester United wameanza kukata pochi kwa ajili ya kuliimarisha jeshi lao baada ya leo Jumatano jioni kumsajili beki wa kati wa Benfica ya Ureno Msweden,Victor Lindelof.

    Lindelof mwenye umri wa miaka 22 amejiunga na Manchester United kwa mkataba wa miaka minne wenye kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi baada ya mapema mchana kufuzu vipimo vyake vya afya.

    Taarifa zaidi zinasema Lindelof amejiunga na Manchester United kwa ada ya uhamisho ya €35m ambayo itapata na kufika €45m iwapo ataonyesha kiwango bora cha uchezaji uwanjani.



    Lindelof alianzia safari yake ya soka kwa kujiunga na klabu ndogo ya Vasteras SK iliyokuwa umbali umbali wa kilomita 100 kutoka mji mkuu wa nchi ya Sweden wa Stockholm.Aliijiunga na kikosi cha kwanza mwaka 2010.

    Disembea 2011 Lindelof alisaini mkataba wa miaka mitano wa kujiunga na kikosi cha Benfica B alichodumu nacho kwa kipindi cha miaka mitatu kabla ya kujiunga na kikosi cha wakubwa.

    Akiwa na kikosi cha wakubwa cha Benfica,Lindelof alifanikiwa kushinda ubingwa wa ligi kuu ya Ureno mara tatu pamoja na kupata nafasi ya kucheza michezo ya klabu bingwa Ulaya.

    Lindelof amekuwa ni mchezaji wa kwanza kujiunga na Manchester United katika kipindi cha majira haya ya joto na atarajiwa kuona kuonekana uwanjani mwezi ujao katika ziara ya michezo ya kujiandaa na msimu mpya itakayofanyika huko Marekani.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Manchester United yafungua usajili yamwaga noti za maana kwa beki wa Benfica Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top