728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, June 14, 2017

    Nyie endeleeni kuwa mikono ya birika tu wenzenu Bayern Munich wanasajili tu


    Munich,Ujerumani.

    MABINGWA wa kihistoria wa ligi ya Bundesliga Bayern Munich wameendelea kukiongezea makali kikosi chao baada ya jioni ya leo kumsajili kiungo wa kati wa Olympique Lyonnais ya Ufaransa,Corentin Tolisso.

    Tolisso mwenye umri wa miaka 22 amesaini mkataba wa miaka mitano wa kuichezea Bayern Munich baada ya Olympique Lyonnais kukubali ada ya uhamisho ya €41.5m.

    Kutua Bayern Munich kwa Tolisso ni pigo kwa vilabu vya Chelsea, Manchester City, Tottenham na Juventus ambavyo pia vilionyesha nia ya kumtaka kiungo huyo aliyefunga mabao 14 msimu uliopita.

    Mara ya mwisho Bayern Munich na Olympique Lyonnais kuuziana wachezaji ilikuwa ni mwaka 2003 pale Bayern Munich ilipomruhusu mshambuliaji wake mahiri wakati huo Giovane Élber kuhamia Olympique Lyonnais.

    Tolisso anakuwa mchezaji wa tatu kujiunga na Bayern Munich katika siku za hivi karibuni baada ya Serge Gnabry aliyetokea Werder Bremen na Niklas Sule aliyetokea Hoffenheim. 


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Nyie endeleeni kuwa mikono ya birika tu wenzenu Bayern Munich wanasajili tu Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top