Michuano ya SportPesa Super Cup inatarajiwa kuanza kutimua vumbi kesho Jumatatu katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam kwa michezo miwili kuchezwa, huku Yanga ikiwa na sura tatu mpya katika kikosi chake.
Mshambuliaji kipenzi cha wana Yanga Mrisho Ngasa aliyekua akiitumikia klabu ya Mbeya City msimu uliopita, amejiunga na kikosi cha Yanga sambamba na winga Haruna Chanongo kutoka Mtibwa Sugar, huku mlinzi wa kati Babu Seif Ally kutoka Kagera Sugar akikamilisha idadi ya sura tatu mpya kambini.
Yanga itawakosa wachezaji wake golikipa Beno Kakolanya, Hassan Kessy, Saimon Msuva, Thaban Kamusoko, Haruna Niyonzima na Amissi Tambwe walio kwenye majukumu ya timu zao za Taifa, na sasa mapengo yao yanaonekana kuzibwa na wachezaji hao waliojiunga kambini na kikosi cha Yanga jana Jumamosi.
Michuano hiyo ya SportPesa Super Cup inashirikisha timu nane, nne kutoka Tanzania na nne kutoka nchini Kenya, ambapo mshindi atacheza na timu ya Everton kutoka Uingereza Julai 13 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
Timu zinazoshiriki michuano hiyo ni Taifa Jang’ombe, Singida United, Simba na Yanga (Tanzania) huku AFC Leoprads, Gor Mahia, Tusker na Nakuru All Stars zikitokea nchini Kenya.
Kesho Jumatatu mchezo wa kwanza utakua kati ya AFC Leopards v Singida Uunited saa 8:00 mchana, Yanga v Tusker saa 10:15 jioni.
Jumanne tarehe 06 Junie, Simba v Nakuru saa 8:00 mchana, Gor Mahia v Taifa Jang’ombe saa 10:15 jioni.
0 comments:
Post a Comment