728x90 AdSpace

Monday, June 12, 2017

AFCON:Misri yadundwa ugenini,yaburuza mkia kwenye kundi lake


Tunis,Tunisia.

MABINGWA wa kihistoria wa Afrika,Misri wameanza kinyonge safari yao ya kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya Afrika (AFCON) ya mwaka 2019 baada ya Jumapili usiku wakiwa ugenini kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa wenyeji wao Tunisia katika mchezo mkali wa kundi J uliofanyika kwenye uwanja wa Rhades jijini Tunis.

Bao lililoikata upepo Misri limefungwa katika dakika ya 49 na mshambuliaji Yassine Yassine aliyetumia vyema pasi ya Ben Youssef.

Kichapo hicho kimeipeleka Misri mkiani mwa kundi J nyuma na Tunisia yenye pointi tatu na Niger pamoja na Swaziland zenye pointi moja moja baada ya Jumamosi jioni kutoka sare ya bila kufungana.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: AFCON:Misri yadundwa ugenini,yaburuza mkia kwenye kundi lake Rating: 5 Reviewed By: Unknown